Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Friday, June 20, 2025

 

SKAUTI NI NINI NA LENGO LAKE NI LIPI?

Chama cha skauti ni chama cha kielimu  chenye malengo ya kumkuza kijana kiimani, kiakili, kijami na kimwili kupitia shughuli mbali mbali kwa kutumia mbinu za kiskauti (scout methods) ili kuijenga dunia iliyo bora  zaidi (creating a better world)Skauti ni chama cha malezi ya vijana, hakihusiani na vyama vya siasa wala dini  na nichama kinachotoa elimu isiyo rasm (non-formal education).

Ni chama cha kielimu cha  hiari na cha kujitolea  kwa vijana wote bila ubaguzi wa aina yoyote ile yaani rangi, kabila, jinsi , dini  au  itikadi. Chama cha skauti Tanzania kilianzishwa mwaka 1912 kikiwa na lengo lile lile la kumwandaa   kijana kielimu  na kumfanya aweze kujitegemea  na aweze kukabiliana na changamoto mbalimbali anazokumbana nazo katika jamii  inayomzunguka   na kuzitatua  na kuwa msaada  wa kutegemewa na jamii husika.

Lengo la skauti ni kuchangia Elimu ya kijana kwa kuiongezea thamni kupitia Ahadi na kanuni za skauti, lakini pia kusaidia kuifanya dunia kuwa mahala bora kwa kuishi Ili kufikia lengo kuu la Skauti”Creating a better World – Kuifanya Dunia kuwa Bora”, Uskauti huendeshwa kwa kuzingatia mbinu kuu saba ambazo kwa wengine hueleweka kama mfumo endelevu wa kujifunzia / kufundishia (Youth program/progressive scheme) ambao Skauti hutumia.

MASHINDANO YA SKAUTI – NGAZI YA MKOA (DAR ES SALAAM)

Madhumuni ya Mashindano haya kwa Vijana wa Skauti

Mashindano ya Skauti ni jukwaa muhimu la kukuza ushindani chanya, kuonesha maarifa ya Skauti, na kujenga mshikamano miongoni mwa vijana kutoka vikosi mbalimbali. Kupitia mashindano haya, vijana hupata fursa ya kutumia kwa vitendo mafunzo yao ya Skauti, kuonyesha ujuzi waliojifunza katika mazingira halisi, na kujifunza kutoka kwa wenzao. Pia ni nafasi muhimu ya kukuza vipaji, nidhamu, uzalendo, na kuandaa vijana kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.


WILAYA YA UBUNGO YANG’ARA MASHINDANO YA MIKOA YA DAR ES SALAAM

Mashindano ya Skauti ya ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam yalifanyika kuanzia tarehe 13 hadi 16 Juni 2025 katika shule ya sekondari Nguva, wilayani Kigamboni. Wilaya ya Ubungo iliwakilishwa na vikosi bora kutoka ngazi zote: Junior Scouts, Senior Scouts, na Rovers, ambao waliandaliwa kwa umahiri mkubwa.

Maandalizi ya mashindano haya yalihusisha tathmini ya vikosi, mafunzo ya nadharia na vitendo, pamoja na maandalizi ya vifaa muhimu. Vijana walipata mafunzo ya kina kuhusu stadi za Skauti ikiwemo kupiga kambi, kupika kisayansi, kufunga mafundo (knots), na ujenzi wa miundo ya mbao (pioneering). Viongozi waliwajengea vijana uwezo wa ushindani, nidhamu, na ujasiri mkubwa.

Katika mashindano hayo, Wilaya ya Ubungo iling’ara kwa namna ya kipekee, ikinyakua nafasi za juu katika makundi yote:

✅ Junior Boys – Ubungo 1


Junior Girls – Ubungo 1


✅ Senior Boys – Ubungo 1



✅ Senior Girls – Ubungo 1


Rover Boys – Ubungo 1


Rover Girls – Ubungo 2


Na zaidi, Patrol ya Traore (Rover Boys) ilitajwa rasmi kama Kikosi Bora cha Mkoa — jambo la heshima kubwa kwa Wilaya ya Ubungo. Kwa jumla, Ubungo iliibuka kuwa Washindi wa Jumla wa Mkoa wa Dar es Salaam, mafanikio ya kihistoria na ya kujivunia.

🎉 PONGEZI KWA KIONGOZI BORA WA PATROL YA WASICHANA – HUSNA TIZO! 🎉

Tunajivunia kutangazwa kuwa Patrol Leader Bora kwa Wasichana katika Mashindano ya Skauti ya Mkoa wa Dar es Salaam ni HUSNA TIZO kutoka Wilaya ya Ubungo! 🏅👏

Husna amethibitisha kuwa uongozi si jina tu, bali ni matendo. Uwezo wake wa kuwaongoza wenzake kwa nidhamu, mshikamano, na ufanisi umemvunia heshima hii kubwa mbele ya Wilaya zote.

Tunaamini Husna ni mfano bora wa kuigwa kwa Skauti wengine na ni ushahidi hai wa matunda ya mafunzo bora ya Skauti katika Wilaya ya Ubungo.

WITO KWA JAMII YA UBUNGO NA SKAUTI TANZANIA

Ushindi huu ni matokeo ya juhudi za pamoja kutoka kwa vijana, viongozi, wazazi, na wadau mbalimbali. Tunatoa pongezi kwa kila mmoja aliyechangia kufanikisha ushindi huu. Ni wakati sasa wa kujiandaa kwa ajili ya mashindano ya Kitaifa. Tunatoa wito kwa jamii nzima kuendelea kuunga mkono harakati hizi kwa hali na mali.

Kwa pamoja, tunaweza kuipeleka Skauti Wilaya ya Ubungo na Tanzania kwa ujumla katika viwango vya juu kitaifa na kimataifa!


MATUKIO KATIKA PICHA












#SkautiNiMaisha
#UbungoInang’ara
#MashindanoYaSkauti2025
#ScoutProudTanzania

Sunday, April 27, 2025


  

Idara ya Programu za Vijana kwa kushirikiana na Idara ya Mafunzo, inaendelea na mazoezi ya maandalizi ya Kambi ya Kielimu (Mashindano) kwa ngazi ya mkoa, yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu.

Mazoezi haya, ambayo yalianza awali mnamo tarehe 7 April 2025, yameendelea mnamo tarehe 27 Aprili 2025, kwa kasi na weledi zaidi, yakilenga kuwaandaa washiriki kwa kina ili kuwajenga kimwili, kiakili, na kimaadili. Lengo ni kuhakikisha washiriki wanakuwa na maandalizi bora yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu na kwa ushindani mkubwa katika mashindano hayo, huku wakizingatia nidhamu ya hali ya juu, mshikamano, na ushindani.

Mazoezi haya yanafanyika kila mwisho wa wiki, siku ya Jumamosi, ambapo washiriki wanapitia programu mbalimbali za:

  • Mazoezi ya viungo,
  • Mafundisho ya uongozi kwa njia ya vitendo na nadharia.

Kupitia mfumo huu, washiriki wanajengewa uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja, kushindana kwa heshima, na kukuza maarifa yao ya msingi katika maeneo mbalimbali ya skauti.

Maandalizi haya yamewahusisha kwa ukamilifu makundi yote ya kambi, ambayo ni:

  • Junior Scouts (wavulana na wasichana),
  • Senior Scouts (wavulana na wasichana),
  • Rover Scouts (wavulana na wasichana).

Vikosi hivi vinaendelea kuundwa kwa kuzingatia vigezo vya ushiriki, nidhamu, na hali ya utayari wa mshiriki mmoja mmoja. Viongozi wa vikundi nao wanashiriki kikamilifu katika mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao wa uongozi na usimamizi wa timu zao.

Kwa pamoja, tunatarajia kuwa kupitia muendelezo huu wa maandalizi ya kina, Wilaya yetu itaweza kuibuka na ushindi wa heshima katika mashindano yajayo, huku tukikuza ari, mshikamano, na maadili mema miongoni mwa vijana wetu.

Kwa Mawasiliano / Maelekezo piga au tuma SMS au WhatsApp 0747724716 | 0740222111

    

 

Imetolewa na 

Idara ya Program za Vijana, Watuwa zima na Mafunzo

Wilaya ya ubungo.

 


Wednesday, April 9, 2025

ZIARA MAALUM – SHULE KWA SHULE


 

Uongozi wa Skauti Wilaya ya Ubungo unatarajia kufanya ziara maalum ya kutembelea shule zote ndani ya Wilaya ya Ubungo kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2025, kwa lengo la kutathmini maendeleo na utekelezaji wa shughuli za Skauti shuleni.

Ziara hii ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha na kufufua shughuli za Skauti katika ngazi ya shule, sambamba na kuhakikisha kuwa miongozo ya malezi ya vijana kupitia Skauti inatekelezwa kikamilifu kulingana na maadili, kanuni, na dira ya Skauti Tanzania.

Katika ziara hii, viongozi wa Skauti watakutana na walimu walezi wa Skauti, viongozi wa vikundi, pamoja na Skauti wenyewe kwa ajili ya:

  • Kufuatilia mwenendo wa programu za Skauti katika shule husika,
  • Kuhamasisha ushiriki mpana wa wanafunzi katika shughuli za Skauti,
  • Kugundua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya Skauti shuleni,
  • Kutoa miongozo, ushauri na motisha kwa vikundi vya Skauti vilivyopo,
  • Kuratibu maandalizi ya mashindano na kambi za wilaya na mkoa.

Aidha, ziara hii inalenga kuimarisha mahusiano kati ya Skauti, shule na jamii, na pia kutoa fursa ya kutambua shule zinazofanya vizuri na kuhamasisha shule nyingine kuongeza juhudi katika uendeshaji wa shughuli za Skauti.

Uongozi wa Skauti wilaya unatoa wito kwa walimu walezi, viongozi wa shule, na wanafunzi wote kushirikiana kwa karibu na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakati wa ziara ili kufanikisha lengo la kuendeleza vijana wenye nidhamu, uwezo wa uongozi, na uzalendo kwa Taifa.

MAANDALIZI YA KAMBI YA MASHINDANO


Idara ya Programu za Vijana kwa kushirikiana na Idara ya Mafunzo, mnamo tarehe 7 Aprili 2025, wameanza rasmi kuendesha mazoezi ya maandalizi ya Kambi ya Kielimu (Mashindano) kwa ngazi ya mkoa, ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu.

Hatua hii muhimu inalenga kuwaandaa washiriki kwa kina, kuhakikisha kuwa wanajengwa vyema kimwili, kiakili, na kimaadili ili waweze kushiriki kikamilifu na kwa ushindani katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika kwa hamasa kubwa, nidhamu ya hali ya juu, na ushindani wa kitaaluma.

Mazoezi haya yatafanyika kila mwisho wa wiki, siku ya Jumamosi, ambapo washiriki watapitia programu mbalimbali za mafunzo, mazoezi ya viungo, mafundisho ya kitaaluma, na mafunzo ya uongozi kwa njia ya vitendo na nadharia. Kupitia mfumo huu, washiriki wanajengewa uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja, kushindana kwa heshima, na kukuza maarifa yao ya msingi katika maeneo mbalimbali ya skauti.

Maandalizi haya yamewalenga makundi yote ya kambi kwa ukamilifu, yakiwemo:

  • Junior Scouts (wavulana na wasichana),
  • Senior Scouts (wavulana na wasichana),
  • Rover Scouts (wavulana na wasichana).

Vikosi hivi vitaundwa kwa kuzingatia vigezo vya ushiriki, nidhamu, na hali ya utayari ya mshiriki mmoja mmoja. Pia, viongozi wa vikundi wanashiriki katika mafunzo haya kuhakikisha wanaimarika katika uongozi na usimamizi wa timu zao ipasavyo.

Kwa pamoja, tunatarajia kuwa kupitia maandalizi haya ya kina, Wilaya yetu itaweza kuibuka na ushindi wa heshima katika mashindano yajayo, huku tukikuza ari, mshikamano, na maadili mema miongoni mwa vijana wetu.

 

 

 

Sunday, March 23, 2025

 Mafunzo ya Awali ya Uongozi (PTC)

Ubungo Local Scouts Association imeandaa Mafunzo ya Awali ya Uongozi (PTC). Mafunzo haya yatafanyika kuanzia tarehe 16 mpaka 19 April 2025
Mafunzo ya awali ya Uongozi wa Skauti ni mafunzo kwa ajili ya watu wazima wenye umri wa kuanzia miaka 18 (Rovers) walio tayari kujiunga au kusaidia kuendesha shughuli za Skauti kwa nyadhifa mbali mbali. Mafunzo haya yatawapa mwongozo wa kuweza kuufahamu u-Skauti na jinsi ya kuweza kusimamia na kuendesha shughuli mbali mbali za Skauti popote watakapo kuwepo.
 
Madhumuni ya mafunzo ya awali ni kama ifuatavyo;
1.      Kupanua ufahamu kuhusu uskauti na shughuli zake.
2.      Kumpatia  Mshiriki stadi katika fani na mafunzo ya kiskauti.
3.      Kukuza hamasa ili apende masuala ya Skauti na Chama Cha Skauti.
4.      Kumhamasisha mshiriki  ili aweze kuwa tayari kujituma na kujitolea katika shughuli za skauti katika wadhifa atakaopewa katika chama cha Skauti.

Mafunzo haya ni mafunzo ya maalumu kwa ajili ya watu wazima wanaotaka kusaidia kuendesha uskauti. Baada ya mafunzo haya, mshiriki anaweza kujiendeleza kwa kushiriki mafunzo ya juu zaidi ya Uongozi wa skauti ambayo yatamfanya awe kiongozi aliyefuzu yaani Skauta.

Kwa kawaida mafunzo haya huitwa mwanzo wa mafunzo ya uongozi (Preliminary Training Course) na huendeshwa kwa mtindo wa  washiriki kuishi kambini kwa muda wa siku tatu au nne. Humo kambini washiriki wataishi pamoja ikiwa ni pamoja na kulala, kupika, na kula. Vilevile watashiriki shughuli zote za mafunzo wakiwa katika vikosi vya watu kati ya  6 na 8 kwa kila kikosi.

Mhitimu wa mafunzo haya hupaswa kuendesha kundi la skauti chini ya usimamizi wa Skauta kwa kipindi kisichopungua miezi sita na akipenda kujiendeleza atapaswa kuhudhuria mafunzo ya Nishani ya Skauta (Wood badge Training Course) ambayo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni nadharia, kambini na vitendo.

Kiutaratibu, mafunzo haya huendeshwa na Mkufunzi yaani Leader Trainer au Mkufunzi Msaidizi ambaye huitwa Assistant Leader Trainer. Lengo la kuwatumia wakufunzi na wakufunzi wasaidizi ni kuhakikisha kuwa vipengele vyote muhimu vanatekelezwa ili kuwafanya washiriki waufahamu na kuuelewa vyema uskauti kwa nadharia na kwa vitendo.

Washiriki wanatakiwa kuthbiitisha ushiriki mapema kwa kuanza kulipia Ada (Unaruhusiwa kulipia kidogo kidogo) kabla ya tarehe 10 April 2025

Kwa Mawasiliano / Maelekezo piga au tuma SMS au WhatsApp 0747724716 | 0740222111
    

Imetolewa na 
Idara ya Program za Vijana, Watuwazima na Mafunzo
Wilaya ya ubungo.

Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi

 


Rova Skauti wilaya ya Ubungo mnamo tarehe 20/03/2025 wametembelea shule ya Sekondari Mburahati, ikiwa ni katika utekelezaji wa mikakati ya Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi unaotekelezwa na Rova 04, Wanaowania Nishani ya Raisi. (President Scout Badge).

Mradi wa huu wa Skauti Wilaya ya Ubungo wenye lengo la Kuimarisha Afya ya Uzazi ni juhudi maalum inayolenga kuwajengea vijana uelewa na stadi za afya ya uzazi kwa lengo la kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla. Mradi huo, unaofadhiliwa na Africa Scout Foundation, unatekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu katika Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam. Uzinduzi rasmi ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Skauti(Upanga dsm). 


Picha ya pamoja Mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi

 Darasa likiendelea wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi



Matukio katika picha Katika shule ya Sekondari Mburahati.

Picha ya pamoja Mara baada ya Darasa kuhusu Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi




 Darasa likiendelea kwa wanafunzi Skauti wa Shule ya Sekondari Mburahati
kuhusu Elimu juu ya Afya ya Uzazi


Wednesday, October 2, 2019

ZIARA MAALUM - SHULEKWA SHULE


Kamishna wa Skauti wilaya ya Ubungo atafanya ziara ya kutembelea shule zote za wialaya ya Ubungo na kutathmini utekelezaji wa shughuli za Skauti shuleni, kuanzia tarehe 1 - 31 Oktoba 2019 



UBUNGO PRILIMINARY TRAING COURSE


Chama cha skauti Tanzania Wilaya aya Ubungo wameandaa mafunzo ya awali ya uongozi wa skauti. Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 4 Novemba 2019 katika eneo la Silver Sand Beach - Kunduchi. Eidha kamishna wa Skauti Wilaya ya Ubungo amesisitiza kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana katika kuongeza idadi ya viongozi wa Skauti lakini pia kupata viongozi walio bora. Gharamaza mafunzo hayo ni Tsh 30,000/- kwa kilamshiriki, 

MADHUMUNI YA MAFUNZO:
  1. Kuwapa mbinu na uwezo wa kuratibu na kusimamia programu za skauti shuleni
  2. kujifunza mbinu za ulinzi na uslama wa mtoto, mahitaji, matarajio, changamoto wanazozikabili na jinsi ya kuzitatua.
  3. Kumfundisha mtoto dhana ya kujitolea kwa kusaidia jamii, utii, uzalendo, ujasiri, ukakamavu na utulivu kwa kupitia programu za vijana.
  4. Kutambua tabia za watoto/vijana ili waweze kuwasaidia kujirekebisha.
  5. Kuondoa tatizo la utoro, utovu wa nidhamu shuleni kwa kutumia mafunzo ya stadi za maisha.
Kasmishna wa skauti ametoa wito kwa wale wote ambao wanastahili kushiriki mafunzo hayo ikiwemo walimu walezi wa skauti mashuleni kujitokeza kwa wingi ili kupata mafunzo hayo muhimu kwa mustakbali wa  chama cha skauti na Taifa letu kwaujumla.



Tuesday, May 7, 2019

MASHINDANO YA SKAUTI NGAZI YA WILAYA NA JUKWAA LA VIJANA LA KWANZA WILAYA YA UBUNGO.


Kwa kuzingatia kalenda ya shuguli za chama ngazi ya Wilaya kwa mwaka 2019, kama ilivyo ada, kutakuwa na mashindano ngazi ya wilaya. Lengo ni kuinua vipaji katika stadi za kiskauti na kupata wawakilishi wa kuwakilisha Wilaya katika mashindano ya Skauti ya Mkoa June 2019.



 
 
 
This Blog Powerd by:
  Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of  Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
murtadhwa@hotmail.com & murtadhaalbahsan@gmail.com
Dar Es Salaam, Tanzania