Uongozi wa Skauti Wilaya ya Ubungo unatarajia kufanya ziara
maalum ya kutembelea shule zote ndani ya Wilaya ya Ubungo kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2025, kwa lengo la kutathmini maendeleo na utekelezaji wa
shughuli za Skauti shuleni.
Ziara hii ni sehemu ya mkakati wa
kuimarisha na kufufua shughuli za Skauti katika ngazi ya shule, sambamba na
kuhakikisha kuwa miongozo ya malezi ya vijana kupitia Skauti inatekelezwa
kikamilifu kulingana na maadili, kanuni, na dira ya Skauti Tanzania.
Katika ziara hii, viongozi wa Skauti
watakutana na walimu walezi wa Skauti, viongozi wa vikundi, pamoja na Skauti
wenyewe kwa ajili ya:
- Kufuatilia mwenendo wa programu za Skauti katika shule
husika,
- Kuhamasisha ushiriki mpana wa wanafunzi katika shughuli
za Skauti,
- Kugundua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya Skauti
shuleni,
- Kutoa miongozo, ushauri na motisha kwa vikundi vya
Skauti vilivyopo,
- Kuratibu maandalizi ya mashindano na kambi za wilaya na
mkoa.
Aidha, ziara hii inalenga kuimarisha
mahusiano kati ya Skauti, shule na jamii, na pia kutoa fursa ya kutambua
shule zinazofanya vizuri na kuhamasisha shule nyingine kuongeza juhudi katika
uendeshaji wa shughuli za Skauti.
Uongozi wa Skauti wilaya unatoa wito
kwa walimu walezi, viongozi wa shule, na wanafunzi wote kushirikiana kwa
karibu na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakati wa ziara ili kufanikisha
lengo la kuendeleza vijana wenye nidhamu, uwezo wa uongozi, na uzalendo kwa
Taifa.
No comments:
Post a Comment