Rova Skauti wilaya ya
Ubungo mnamo tarehe 20/03/2025 wametembelea shule ya Sekondari Mburahati, ikiwa
ni katika utekelezaji wa mikakati ya Mradi
wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi unaotekelezwa na Rova 04, Wanaowania Nishani
ya Raisi. (President Scout Badge).
Mradi wa huu wa Skauti Wilaya ya Ubungo wenye lengo la
Kuimarisha Afya ya Uzazi ni juhudi maalum inayolenga kuwajengea vijana uelewa
na stadi za afya ya uzazi kwa lengo la kuboresha maisha yao na jamii kwa
ujumla. Mradi huo, unaofadhiliwa na Africa
Scout Foundation, unatekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu katika Wilaya
ya Ubungo, Dar es Salaam. Uzinduzi rasmi ulifanyika katika ofisi za makao makuu
ya Skauti(Upanga dsm).
![]() |
Picha ya pamoja Mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi |
![]() |
Darasa likiendelea wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi |
Matukio katika picha Katika shule ya Sekondari Mburahati.
![]() |
Picha ya pamoja Mara baada ya Darasa kuhusu Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi |
![]() |
Darasa likiendelea kwa wanafunzi Skauti wa Shule ya Sekondari Mburahati kuhusu Elimu juu ya Afya ya Uzazi |
No comments:
Post a Comment