SKAUTI NI NINI NA LENGO LAKE NI LIPI?
MASHINDANO YA SKAUTI – NGAZI YA MKOA (DAR ES SALAAM)
Madhumuni ya Mashindano haya kwa Vijana wa Skauti
Mashindano ya Skauti ni jukwaa muhimu la kukuza ushindani chanya, kuonesha maarifa ya Skauti, na kujenga mshikamano miongoni mwa vijana kutoka vikosi mbalimbali. Kupitia mashindano haya, vijana hupata fursa ya kutumia kwa vitendo mafunzo yao ya Skauti, kuonyesha ujuzi waliojifunza katika mazingira halisi, na kujifunza kutoka kwa wenzao. Pia ni nafasi muhimu ya kukuza vipaji, nidhamu, uzalendo, na kuandaa vijana kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
WILAYA YA UBUNGO YANG’ARA MASHINDANO YA MIKOA YA DAR ES SALAAM
Mashindano ya Skauti ya ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam yalifanyika kuanzia tarehe 13 hadi 16 Juni 2025 katika shule ya sekondari Nguva, wilayani Kigamboni. Wilaya ya Ubungo iliwakilishwa na vikosi bora kutoka ngazi zote: Junior Scouts, Senior Scouts, na Rovers, ambao waliandaliwa kwa umahiri mkubwa.
Maandalizi ya mashindano haya yalihusisha tathmini ya vikosi, mafunzo ya nadharia na vitendo, pamoja na maandalizi ya vifaa muhimu. Vijana walipata mafunzo ya kina kuhusu stadi za Skauti ikiwemo kupiga kambi, kupika kisayansi, kufunga mafundo (knots), na ujenzi wa miundo ya mbao (pioneering). Viongozi waliwajengea vijana uwezo wa ushindani, nidhamu, na ujasiri mkubwa.
Katika mashindano hayo, Wilaya ya Ubungo iling’ara kwa namna ya kipekee, ikinyakua nafasi za juu katika makundi yote:
✅ Junior Boys – Ubungo 1
✅ Junior Girls – Ubungo 1
✅ Senior Boys – Ubungo 1
✅ Rover Girls – Ubungo 2
Na zaidi, Patrol ya Traore (Rover Boys) ilitajwa rasmi kama Kikosi Bora cha Mkoa — jambo la heshima kubwa kwa Wilaya ya Ubungo. Kwa jumla, Ubungo iliibuka kuwa Washindi wa Jumla wa Mkoa wa Dar es Salaam, mafanikio ya kihistoria na ya kujivunia.
🎉 PONGEZI KWA KIONGOZI BORA WA PATROL YA WASICHANA – HUSNA TIZO! 🎉
Tunajivunia kutangazwa kuwa Patrol Leader Bora kwa Wasichana katika Mashindano ya Skauti ya Mkoa wa Dar es Salaam ni HUSNA TIZO kutoka Wilaya ya Ubungo! 🏅👏
Husna amethibitisha kuwa uongozi si jina tu, bali ni matendo. Uwezo wake wa kuwaongoza wenzake kwa nidhamu, mshikamano, na ufanisi umemvunia heshima hii kubwa mbele ya Wilaya zote.
Tunaamini Husna ni mfano bora wa kuigwa kwa Skauti wengine na ni ushahidi hai wa matunda ya mafunzo bora ya Skauti katika Wilaya ya Ubungo.
WITO KWA JAMII YA UBUNGO NA SKAUTI TANZANIA
Ushindi huu ni matokeo ya juhudi za pamoja kutoka kwa vijana, viongozi, wazazi, na wadau mbalimbali. Tunatoa pongezi kwa kila mmoja aliyechangia kufanikisha ushindi huu. Ni wakati sasa wa kujiandaa kwa ajili ya mashindano ya Kitaifa. Tunatoa wito kwa jamii nzima kuendelea kuunga mkono harakati hizi kwa hali na mali.
Kwa pamoja, tunaweza kuipeleka Skauti Wilaya ya Ubungo na Tanzania kwa ujumla katika viwango vya juu kitaifa na kimataifa!
MATUKIO KATIKA PICHA
#SkautiNiMaisha
#UbungoInang’ara
#MashindanoYaSkauti2025
#ScoutProudTanzania
No comments:
Post a Comment