Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Sunday, April 27, 2025


  

Idara ya Programu za Vijana kwa kushirikiana na Idara ya Mafunzo, inaendelea na mazoezi ya maandalizi ya Kambi ya Kielimu (Mashindano) kwa ngazi ya mkoa, yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu.

Mazoezi haya, ambayo yalianza awali mnamo tarehe 7 April 2025, yameendelea mnamo tarehe 27 Aprili 2025, kwa kasi na weledi zaidi, yakilenga kuwaandaa washiriki kwa kina ili kuwajenga kimwili, kiakili, na kimaadili. Lengo ni kuhakikisha washiriki wanakuwa na maandalizi bora yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu na kwa ushindani mkubwa katika mashindano hayo, huku wakizingatia nidhamu ya hali ya juu, mshikamano, na ushindani.

Mazoezi haya yanafanyika kila mwisho wa wiki, siku ya Jumamosi, ambapo washiriki wanapitia programu mbalimbali za:

  • Mazoezi ya viungo,
  • Mafundisho ya uongozi kwa njia ya vitendo na nadharia.

Kupitia mfumo huu, washiriki wanajengewa uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja, kushindana kwa heshima, na kukuza maarifa yao ya msingi katika maeneo mbalimbali ya skauti.

Maandalizi haya yamewahusisha kwa ukamilifu makundi yote ya kambi, ambayo ni:

  • Junior Scouts (wavulana na wasichana),
  • Senior Scouts (wavulana na wasichana),
  • Rover Scouts (wavulana na wasichana).

Vikosi hivi vinaendelea kuundwa kwa kuzingatia vigezo vya ushiriki, nidhamu, na hali ya utayari wa mshiriki mmoja mmoja. Viongozi wa vikundi nao wanashiriki kikamilifu katika mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao wa uongozi na usimamizi wa timu zao.

Kwa pamoja, tunatarajia kuwa kupitia muendelezo huu wa maandalizi ya kina, Wilaya yetu itaweza kuibuka na ushindi wa heshima katika mashindano yajayo, huku tukikuza ari, mshikamano, na maadili mema miongoni mwa vijana wetu.

Kwa Mawasiliano / Maelekezo piga au tuma SMS au WhatsApp 0747724716 | 0740222111

    

 

Imetolewa na 

Idara ya Program za Vijana, Watuwa zima na Mafunzo

Wilaya ya ubungo.

 


No comments:

Post a Comment