1.1.
Utanngulizi.
Chama cha skauti ni chama cha kielimu chenye malengo ya kumkuza kijana kiimani,
kiakili, kijami na kimwili kupitia shughuli mbali mbali kwa kutumia mbinu za
kiskauti (scout methods) ili
kuijenga dunia iliyo bora zaidi (creating a better world). Skauti ni chama cha malezi
ya vijana, hakihusiani na vyama vya siasa wala dini na nichama kinachotoa elimu isiyo rasm (non-formal education).
Ni
chama cha kielimu cha hiari na cha
kujitolea kwa vijana wote bila ubaguzi
wa aina yoyote ile yaani rangi, kabila, jinsi , dini au itikadi. Chama cha skauti Tanzania kilianzishwa mwaka 1912
kikiwa na lengo lile lile la kumwandaa kijana kielimu
na kumfanya aweze kujitegemea na
aweze kukabiliana na changamoto mbalimbali anazokumbana nazo katika jamii inayomzunguka na kuzitatua
na kuwa msaada wa kutegemewa na
jamii husika.
Lengo la skauti ni kuchangia Elimu ya kijana kwa
kuiongezea thamni kupitia Ahadi na kanuni za skauti, lakini pia kusaidia
kuifanya dunia kuwa mahala bora kwa kuishi Ili kufikia lengo kuu la
Skauti”Creating a better World – Kuifanya Dunia kuwa Bora”, Uskauti huendeshwa
kwa kuzingatia mbinu kuu saba ambazo kwa wengine hueleweka kama mfumo endelevu
wa kujifunzia / kufundishia (Youth program/progressive scheme) ambao Skauti
hutumia.
1.2.
Uongozi wa Skauti ngazi ya Wilaya
Chama cha skauti ngazi ya wilaya kilipata uteuzi wa kwanza wa
kamishna na msaidizi wake mnamo mwaka 2017 mwezi July tangu kuanzishwa kwa
Wilaya mpya ya Ubungo (2015) na kuapishwa rasmi mkoani Dodoma katika maadhimisho
ya miaka 100 ya Skauti nchini. kadhalika mwaka huu 2019 mwezi March Kamishna
Mkuu alifanya uteuzi mpya wa makamishna wakuu wasaidizi pamojana makamishna wa
Mikoa na Wilaya, hivyo aliteua Kamishna na Kamishna Msaidizi wa Wilaya yetu hii
ya Ubungo na kuapishwa rasmi katika ofisi za Makao Makuu ya chama cha Skauti –
Upanga amabao ni Bw. Florence J. Assenga
– Kamishna wa Wilaya na Bw.
Murtadhwa R. Abdallah – Kamishna Msaidizi wa Wilaya. Kama kawaida utaratibu ulivyo ,Uongozi wa Wilaya tumeunda kamati ya Uendeshaji yenye
waratibu takriban 13 katika idara mbali mbali, ili kuunganisha nguvu zetu kwa
lengo la kuendeleza Skauti kwa ufanisi mkubwa
katika Wilaya yetu ya Ubungo.
Bodi ya Skauti ya Wilaya
ndiyo chombo kinachosimamia shughuli za Skauti Wilaya ya Ubungo kwa niaba ya
Baraza la Skauti Taifa, ambapo kwa sasa bado tunaitumia bodi iliyoundwa awali
hadi hapo itakapo fikia wakati wa kufanya uchaguzi mpya wa Bodi nyengine kwa
mujibu wa katiba ya chama cha Skauti Tanzania.
1.3.
IDARA MBALIMBALI ZA
CHAMA NGAZI YA WILAYA - UBUNGO
1.3.1. Idara ya Mipango na Utawala Bora (Administration
and Good Governance /Program)
Ni Idara yenye jukumu la kusimamia shughuli zote za kiofisi ikiwa ni
pamoja na masuala ya mipango na utawala bora na kufuatilia utendaji/uwajibikaji
wa waratibu wote katika Wilaya.
1.3.2. Idara ya Mafunzo na Program za Vijana (Training
and Youth Program)
Idara hii ndio mhimili Wa Wilaya wa Chama. Ni Idara yenye jukumu
la kuandaa Viongozi wote wa Skauti kutoka rika la Kabu, Junior, Senior hadi
Rova Skauti. Idara hii ndio inayoratibu shughuli zote za progamu za Vijana na
kusimamia utekelezwaji wa shughuli hizo katka makundi kwa kuzingatia “Youth
Program” sambamba na kuandaa mashindano ya Skauti kwa makundi mbalimbali ngazi
ya Wilaya, ikihusisha Majukwaa ya Vijana, Semina, na Warsha mbalimbali
zinazohusu program za vijana Skauti. Kuandaa Watahini (Assesors) wa mashindano
n.k.
1.3.3. Idara ya Hati na Usajili (Warranty and
Registration)
Idara hii ndio yenye dhamana na jukumu la kutunza na kuhifadhi
kumbukumbu zote za wanachama wote wa Chama cha Skauti Wilaya ya Ubungo. Idara
hii inasimamia usajili wa wanachama pamja na makundi yote ya skauti wailaya ya
Ubungo sambamba na ulipaji wa ada za uanachama katika Wilaya ya Ubungo.
1.3.4. Idara ya Mawasiliano, Habari, Teknolojia
na JOTA & JOTI. (ICT, and Publication)
Idara hii ndio yenye jukumu la kutunza kumbukumbu za Viongozi wote
wa Skauti waliopo madarakani na ambao wamepita na kushika nyadhifa mbalimbali
katika Chama. Idara hii pia inahusika kuandaa Majarida, Mikutano na Vyombo vya
Habari, (Press Conferences) kurekodi Matukio mbalimbali ya Chama ngazi ya
Wilaya na kuyahifadhi. Kuandaa Mafunzo ya Mawasiliano ya Radio pamoja na masuala
ya ICT kwa Skauti na Viongozi wa Skauti, ikiwa ni pamoja na kuratibu na
kusimamia shughuli ya kila mwaka iitwayo Jamboree ya Hewani ya Skauti
(JOTA-JOTI).
1.3.4. Idara ya Makambi na Mzingira. (Environment, Camp
and Campsite )
Idara hii inahusika kulinda na kutunza Kambi za Skauti tulizonazo.
Lakini kwa kushirkiana na mratibu wa shughuli za skauti ngazi ya wilaya idara
hii inatakiwa kuhakikisha kuwa chama cha skauti
(W) ubungo tunakuwa na maeneo ya makambi kwa ajili ya mafunzo kwa vijana
wetu wa skauti.
1.3.5. Idara ya Hali hatarishi na Uokoaji. (Disaster
Management)
Idara hii ndio inayoratibu shughuli zote za Maafa Wilayani.
Inatakiwa kuandaa mpango mkakati madhubuti wa kujipanga kikamilifu katika
kushiriki kwenye shughuli mbali bali za maafa zitakazo jitokeza wakati wowote
lakini pia kuunda kikosi cha Vijana skauti cha maafa kitakacho kuwa tayari wakati
kitapo hitajika kwa lengo la kutoa huduma.
1.3.6. Idara ya Miradi na Maendeleo ya Jamii.
(Community Development and Out Reach)
Idara hii ndio yenye kazi kubwa ya kutafuta miradi ya uzalishaji
mali na kuingiza kipato kwa Chama. Ili shughuli za Chama ziweze kufanyika
tunahitaji kuwa na pesa za kutosha kukidhi mahitaji ya kila Idara. Idara hii
pia hutoa Mafunzo ya jinsi ya kuanzisha miradi midogo midogo kwa Makundi ya
Skauti ngazi ya wilaya. Inapotokea shughuli kubwa za Chama idara hii huhusika
katika kufanya fund raising mbalimbali ili kukiingizia Chama pesa.
1.4.
Idadi
ya Wanachama
Hadi sasa wilaya ya Ubungo tunakadiria kuwa na wanachama zaidi ya 2,129 (Elfu mbili Mia moja Ishirini na
Tisa) idadi imekuwa ikibadilika kila mwaka kutokana na wale wanao hitimu
kidato cha nne na wale wanaomaliza darasa la saba kila mwaka. Pia kumekuwa na
ongezeko kwa kila mwaka tunafanya usajili kwa ajili ya wanachama wapya
kujiunga.
Tayari tumeshaunda mfumo malum utakaoweza kutupatia na kuhifadhi data
kamili kwa Wilaya yetu ya Ubungo (Membership Database System) ambayo itaonesha
idadi ya Skauti kwa makundi rika yao (Scouts
Section)
Jedwali
hapa chini linaonyesha idadi kwa mfumo wa rika (Scouts Section) kama ifuatavyo;-
s/n
|
Item
|
Sex
|
Subtotal
|
Total
|
1.
|
Cub
|
Boys
|
515
|
1007
|
Girls
|
492
|
|||
2.
|
Junior
|
Boys
|
375
|
802
|
Girls
|
427
|
|||
3.
|
Senior
|
Boys
|
84
|
188
|
Girls
|
104
|
|||
4.
|
Rover
|
Boys
|
93
|
132
|
Girls
|
39
|
|||
5.
|
Grand total
|
2,129
|
1.5.
Idadi
ya Wataalamu/Viongozi (Lt, Alt, Sl na Gsl)
Chama cha skauti wilaya ya Ubungo tuna
makadirio ya viongozi wasio zidi 100 (mia
moja) Makadirio hayo tumeyafanya kwa kupitia viongozi wanao kuja kuomba
usajili wa makundi ya skaut katika wilaya yetu ya Ubungo na wale wanomba
kushiriki katika kozi mbali mbali za ungozi.
Jedwali
hapa chini linaonyesha idadi na ngazi zao (Scouts Rank)
kama ifuatavyo;-
s/n
|
Item
|
Sex
|
Sub
Total
|
Total
|
1.
|
Lt
|
Male
|
2
|
2
|
Female
|
0
|
|||
2.
|
ALT
|
Male
|
5
|
6
|
Female
|
1
|
|||
3.
|
SL
|
Male
|
23
|
32
|
Female
|
9
|
|||
4.
|
GSL
|
Male
|
48
|
60
|
Female
|
12
|
|||
5.
|
Grand total
|
100
|
1.6. SHUKRANI
Tunashukuru uongozi mzima
wa serikali wa halmashauri ya manispaa ya Ubungo yaani Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa manispaa, na
maafisa elimu wote (msingi na sekondari) kwa ushirikiano mkubwa kwa Skauti.
Tunashukuru wakuu wa
shule zote zenye Skauti na wazazi wa maskauti hao kwa kutuwezesha kufanya kazi
zetu katika mazingira rafiki.
Tunashukuru viongozi
wote wa makundi kwa jitihada na kujitoa katika kuwalea maskauti wetu.
Tunashukuru kamishna
wa mkoa wa Dar es salaam na uongozi mzima wa Taifa kwa kutuonyesha dira na
kutuwezesha kukamilisha majukumu yetu kikamilifu.
Mwisho lakini sio
mwisho kwa umuhimu tunatoa shukrani kwa kamati ya Uendeshaji na Bodi ya wilaya
ya Ubungo kwa ushirikiano, kujituma na kujitoa kwao katika kufanikisha majukumu
mbali mbali.
This Blog Powerd by:
Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 623 511 232
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment