Idara ya Programu za Vijana kwa kushirikiana na Idara ya Mafunzo, inaendelea na mazoezi ya maandalizi ya Kambi
ya Kielimu (Mashindano) kwa ngazi ya mkoa, yanayotarajiwa kufanyika
mwezi Juni mwaka huu.
Mazoezi haya, ambayo yalianza awali mnamo tarehe 7 April 2025,
yameendelea mnamo tarehe 27 Aprili 2025, kwa kasi na weledi zaidi, yakilenga
kuwaandaa washiriki kwa kina ili kuwajenga kimwili, kiakili, na kimaadili.
Lengo ni kuhakikisha washiriki wanakuwa na maandalizi bora yatakayowawezesha
kushiriki kikamilifu na kwa ushindani mkubwa katika mashindano hayo, huku
wakizingatia nidhamu ya hali ya juu, mshikamano, na ushindani.
Mazoezi haya yanafanyika kila mwisho wa wiki, siku ya Jumamosi,
ambapo washiriki wanapitia programu mbalimbali za:
- Mazoezi ya viungo,
- Mafundisho ya uongozi kwa njia
ya vitendo na nadharia.
Kupitia mfumo huu, washiriki wanajengewa uwezo wa kufanya kazi kwa
pamoja, kushindana kwa heshima, na kukuza maarifa yao ya msingi katika maeneo
mbalimbali ya skauti.
Maandalizi haya yamewahusisha kwa ukamilifu makundi yote ya kambi,
ambayo ni:
- Junior Scouts (wavulana na wasichana),
- Senior Scouts (wavulana na wasichana),
- Rover Scouts (wavulana na wasichana).
Vikosi hivi vinaendelea kuundwa kwa kuzingatia vigezo vya
ushiriki, nidhamu, na hali ya utayari wa mshiriki mmoja mmoja. Viongozi wa
vikundi nao wanashiriki kikamilifu katika mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao
wa uongozi na usimamizi wa timu zao.
Kwa pamoja, tunatarajia kuwa kupitia muendelezo huu wa maandalizi
ya kina, Wilaya yetu itaweza kuibuka na ushindi wa heshima katika mashindano
yajayo, huku tukikuza ari, mshikamano, na maadili mema miongoni mwa vijana
wetu.
Kwa Mawasiliano / Maelekezo piga au tuma SMS au WhatsApp 0747724716 | 0740222111
Imetolewa na
Idara ya Program za Vijana, Watuwa zima na
Mafunzo
Wilaya ya ubungo.