Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Sunday, March 23, 2025

 Mafunzo ya Awali ya Uongozi (PTC)

Ubungo Local Scouts Association imeandaa Mafunzo ya Awali ya Uongozi (PTC). Mafunzo haya yatafanyika kuanzia tarehe 16 mpaka 19 April 2025
Mafunzo ya awali ya Uongozi wa Skauti ni mafunzo kwa ajili ya watu wazima wenye umri wa kuanzia miaka 18 (Rovers) walio tayari kujiunga au kusaidia kuendesha shughuli za Skauti kwa nyadhifa mbali mbali. Mafunzo haya yatawapa mwongozo wa kuweza kuufahamu u-Skauti na jinsi ya kuweza kusimamia na kuendesha shughuli mbali mbali za Skauti popote watakapo kuwepo.
 
Madhumuni ya mafunzo ya awali ni kama ifuatavyo;
1.      Kupanua ufahamu kuhusu uskauti na shughuli zake.
2.      Kumpatia  Mshiriki stadi katika fani na mafunzo ya kiskauti.
3.      Kukuza hamasa ili apende masuala ya Skauti na Chama Cha Skauti.
4.      Kumhamasisha mshiriki  ili aweze kuwa tayari kujituma na kujitolea katika shughuli za skauti katika wadhifa atakaopewa katika chama cha Skauti.

Mafunzo haya ni mafunzo ya maalumu kwa ajili ya watu wazima wanaotaka kusaidia kuendesha uskauti. Baada ya mafunzo haya, mshiriki anaweza kujiendeleza kwa kushiriki mafunzo ya juu zaidi ya Uongozi wa skauti ambayo yatamfanya awe kiongozi aliyefuzu yaani Skauta.

Kwa kawaida mafunzo haya huitwa mwanzo wa mafunzo ya uongozi (Preliminary Training Course) na huendeshwa kwa mtindo wa  washiriki kuishi kambini kwa muda wa siku tatu au nne. Humo kambini washiriki wataishi pamoja ikiwa ni pamoja na kulala, kupika, na kula. Vilevile watashiriki shughuli zote za mafunzo wakiwa katika vikosi vya watu kati ya  6 na 8 kwa kila kikosi.

Mhitimu wa mafunzo haya hupaswa kuendesha kundi la skauti chini ya usimamizi wa Skauta kwa kipindi kisichopungua miezi sita na akipenda kujiendeleza atapaswa kuhudhuria mafunzo ya Nishani ya Skauta (Wood badge Training Course) ambayo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni nadharia, kambini na vitendo.

Kiutaratibu, mafunzo haya huendeshwa na Mkufunzi yaani Leader Trainer au Mkufunzi Msaidizi ambaye huitwa Assistant Leader Trainer. Lengo la kuwatumia wakufunzi na wakufunzi wasaidizi ni kuhakikisha kuwa vipengele vyote muhimu vanatekelezwa ili kuwafanya washiriki waufahamu na kuuelewa vyema uskauti kwa nadharia na kwa vitendo.

Washiriki wanatakiwa kuthbiitisha ushiriki mapema kwa kuanza kulipia Ada (Unaruhusiwa kulipia kidogo kidogo) kabla ya tarehe 10 April 2025

Kwa Mawasiliano / Maelekezo piga au tuma SMS au WhatsApp 0747724716 | 0740222111
    

Imetolewa na 
Idara ya Program za Vijana, Watuwazima na Mafunzo
Wilaya ya ubungo.

Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi

 


Rova Skauti wilaya ya Ubungo mnamo tarehe 20/03/2025 wametembelea shule ya Sekondari Mburahati, ikiwa ni katika utekelezaji wa mikakati ya Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi unaotekelezwa na Rova 04, Wanaowania Nishani ya Raisi. (President Scout Badge).

Mradi wa huu wa Skauti Wilaya ya Ubungo wenye lengo la Kuimarisha Afya ya Uzazi ni juhudi maalum inayolenga kuwajengea vijana uelewa na stadi za afya ya uzazi kwa lengo la kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla. Mradi huo, unaofadhiliwa na Africa Scout Foundation, unatekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu katika Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam. Uzinduzi rasmi ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Skauti(Upanga dsm). 


Picha ya pamoja Mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi

 Darasa likiendelea wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi



Matukio katika picha Katika shule ya Sekondari Mburahati.

Picha ya pamoja Mara baada ya Darasa kuhusu Mradi wa Elimu juu ya Afya ya Uzazi




 Darasa likiendelea kwa wanafunzi Skauti wa Shule ya Sekondari Mburahati
kuhusu Elimu juu ya Afya ya Uzazi